Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imepata msiba wa
kuondokewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani (Mb) aliyefariki tarehe
24 Septemba, 2015 katika Hospitali ya Apollo nchini India alipokuwa
akipatiwa matibabu.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inatoa pole kwa
familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na Serikali kwa ujumla
kwa kuondokewa na kiongozi mchapakazi, mwadilifu, mzalendo na
aliyekuwa na mapenzi mema na nchi yake.
Wakati wa uhai wake, Mhe. Kombani alijitoa kulitumikia taifa bila
ubaguzi wala upendeleo wowote, hivyo Ofisi itamuenzi kwa kufanya
kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo mbalimbali
katika Utumishi wa Umma kama alivyokuwa akisisitiza.
Mhe. Kombani aliteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma mwaka 2012 akitokea Wizara ya Katiba na
Sheria. Mhe. Kombani amekitumikia cheo hicho mpaka mauti
yalipomfika.
Pumzika kwa Amani mpendwa wetu, Ofisi itaendelea kukukumbuka
daima kwa busara zako na uongozi wako uliotukuka.
Imetolewa Na:
Kaimu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...