THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Serikali ya Awamu ya nne inayomaliza
muda wake mwezi Octoba mwaka huu, imeyashughulikia matatizo yaliyokuwepo kwa
kiasi kikubwa na yale ambayo bado kukamilika, utekelezaji wake unaendelea na
mengine mipango imekwisha anza.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema
hayo jana mjini Kigoma katika uwanja wa Tanganyika, kwenye mkutano wa hadhara
kwa madhumuni ya kuagana na wananchi wa Kigoma.
"Mlinichagua, mlinipa imani
yenu, sikusahau kwa sababu nilikua naifahamu Kigoma, kilio chenu nilikuwa
nakifahamu". Rais
amewaambia wananchi waliofurika uwanjani hapo.
Matatizo yaliyokuwepo Mkoani Kigoma
wakati Rais Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005 ni pamoja na tatizo la umeme
ambapo serikali ilinunua jenereta na kulifunga Mkoani Kigoma.
Jenereta hilo lilitatua matatizo ya
umeme katika miji ya Kasulu, Kibondo na Kigoma Ujiji.
Awamu ya pili ya utatuaji wa matatizo
ya Umeme, yanatatuliwa chini ya Mradi wa Umeme Vijijini, maarufu kama Rural Electrification Agency (REA), ambao
umekua na lengo la kuunganisha vijiji vilivyobakia.
Tayari vijiji 92 vimeunganishwa
na hatimaye vijiji 306 vya Mkoa mzima vitaunganishwa. Awamu hii itahusisha
Ujenzi wa kituo cha kuongeza nguvu ya umeme na hatimaye umeme kufika Wilaya
zingine za Uvinza, Buhigwe na Kakonko.
Tatizo lingine lilokuwepo ni Maji
ambapo Rais Kikwete amesema Mradi mkubwa unaofadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya
unatarajia kukamilika mapema mwakani
Mkoa wa Kigoma pia umekua na tatizo
la Mawasiliano ambapo, mwaka 2005 wakati Rais Kikwete anaingia madarakani, Mkoa
ulikua na barabara moja ya lami yenye urefu wa kilomita 7.36, Hivi sasa kuna
barabara za lami zenye kilomita 28.7 Kigoma mjini, Kasulu kilomita 1.5 na
Kibondo kilomita 2.7.
Mbali na barabara za mjini, serikali
ya awamu ya nne imeunganisha Mkoa wa Kigoma na Mikoa jirani kwa kujenga
barabara kwa kiwango cha lami. Barabara hizo ni za Kigoma-Kidahwe km 28.2,
Mwadiga-Manyovu km 60 na Kidahwe Uvinza km 76.6 na ujenzi ukiwa bado unaendelea
kwa barabara za Kidahwe-Kasulu km 50, Nyakanazi- Kakonko-Kabingo km 75.
Leo tarehe 15 Septemba, Rais Kikwete
anatarajia kuzindua daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi lenye urefu mita
275 na barabara zake unganishi zenye urefu wa km 48. Rais pia atazindua
barabara ya Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa km 76.6 ambayo imejengwa kwa
kiwango cha lami.
Imetolewa
na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-Kigoma
15 Septemba, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...