Rais Jakaya Kikwete akizungumza na washiriki (hawapo pichani) wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kuleta maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa hotuba yake kabla ya kumkaribisha Rais Jakaya Kikwete (kulia meza kuu) katika Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ili aweze kuufungua mkutano huo. Katika hotuba yake Waziri Chikawe alisema mfumo wa utoaji taarifa kwa uwazi umekuwa muhimu kwani unaleta uwazi pamoja na uwajibikaji katika utoaji wa huduma. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 Afrika, unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani Afrika. Wapili kulia meza kuu, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird. Anayefuata ni Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue.
 Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Mfumo wa Takwimu Huria Barani Afrika wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) kwa makini wakati akitoa hotuba yake katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Rais Kikwete alisema jukumu la utoaji wa taarifa kwa umma si kwa serikali pekee bali hata kwa Sekta binafsi pamoja na taasisi zingine zisizokuwa za serikali zinatakiwa kufuata mfumo huo ili kuleta maendeleo katika nchi husika. Mkutano huo ambao unaudhuriwa na mamia ya washiriki kutoka nchi 23 barani Afrika unalengo la kutoa elimu pamoja na kuhamasisha umma kuhusu utoaji wa taarifa kwa uwazi katika sehemu mbalimbali barani humo.
 Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...