Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye hali ya furaha mara baada ya kuzindua msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) ambao ndio warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (mwenye shati jeupe), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa pili kulia) na Bi Ummy Hassan kutoka idara ya Uhusiano NSSF ambao ni moja wa wadhamini wakuu wa mbio hizo.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) warataibu wa mbio hizo Bw Erasto Kilawe (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Novemba 15 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.  Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi  (wa pili kushoto), Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw. Salim Kimaro (wa tatu kushoto).
Na Mwandishi Wetu.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi, amezindua msimu wa saba wa mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika Novemba 15 mwaka huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mbio za Rock City Marathon, zinazoandaliwa na Kampuni ya Capital Plus International (CPI), kwa ushirikiano na Chama cha Riadha Tanzania (RT), pamoja na Chama cha Riadha Mkoa wa Mwanza (MRAA) zinalenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Bw. Malinzi alisema baraza linafuraha kuona makampuni binafsi yakijiingiza katika kuinua mchezo wa riadha nchini.
“Mchezo wa riadha una changamoto kubwa na tunatambua jitihada zinazoendelea kufanywa na kampuni ya Capital Plus katika kurudisha hadhi ya mchezo  huu nchini kama ilivyokuwa miaka ya sabini na themanini,” alisema.
 Alisema kuwa Tanzania itarudi kileleni katika medani za michezo duniani kama wachezaji wataandaliwa katika viwango vinavyokubalika kimataifa.
“Inashangaza kuona taifa la watu milioni 45 linawakilishwa na wanariadha wachache sana, tena katika mbio ndefu huku tukikosa wanariadha wanaoliwakilisha vyema taifa katika mbio fupi,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...