Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard  Membe akihutubia katika ufunguzi rasmi wa Semina ya Ushirikiano wa Kibiashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Norway iliyofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency ya Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Monica Maeland, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Norway nchini, Mhe. Hanna-Marie Kaarstad na wadau wengine katika sekta ya biashara na uwekezaji kutoka Norway na hapa nchini.
Waziri wa Biashara na Viwanda wa Norway, Mhe. Maeland (kulia) akimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo. Kushoto ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula na katikati ni  Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Kaarstad. 
Waziri Membe akiendelea kuzungumza
Waziri wa Biasha na Viwanda nchini Norway Mhe. Monica Maeland naye alipata fursa ya kuzungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya Ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Norway, Mhe. Maeland yupo nchini kwa lengo la kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wa Tanzania nchini Norway. Pia wakati wa ziara hiyo Mhe. Maeland amezindua mtambo wa mbolea wa Yara ulioko kwenye Bandari ya Dar es Salaam na pia atatembelea Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (kulia) na mmoja wa wadau katika semina hiyo Bw. John Ulanga (kushoto) wakifuatilia Hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa na Mhe. Membe na Mhe. Maeland. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...