Kikosi kazi cha Timu ya Tanzania Prisons katika Picha ya
Pamoja leo katika uwanja wa Sokeine Jijini Mbeya katika Mtanange wa
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambapo Timu ya Tanzania Prison
iliibuka mshindi kwa kuwafunga Mbeya City fc Bao moja kwa Sifuri 1-0,
ambapo Mchezaji wa Timu ya Tanzania Prison Jumanne Elfadhili dk ya 32
ndiye aliye ipatia ushindi Timu hiyo ya Tanzania Prison baada ya
kupokea pande kutoka kwa Salum Kimenya.
Golikipa machachari wa Timu ya Tanzania Prisons Aron Kalambo akiwa amedaka
Mpira huku akiwa amezungukwa na Mchezaji wa Timu ya Mbeya City David
Kambole Shoto na Wachezaji Salum Kimenya mwenye Jezi Nambari 14
Mgongoni Sanjari na Jumanne Elfadhili..
Mtanange ukiendelea katika Uwanja wa Sokeine Jijini Mbeya
ambapo Tanzania Prison iliibuka kidedea kwa kuibugiza Mbeya City fc
Goli 1-0.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...