Askali wa usalama barabarani akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule ya za msingi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa navyeti walivyo tunukiwa mara baada ya kupata mafunzo ya usalama barabarani jijini Dar es Salaam.
Na Tom Bishop.
KAMPUNI ya Mafuta ya Tatal Tanzania imedhamini mafunzo ya usalama
barabarani kwa shule za msingi 10 jijini Dar es Salaam.
Udhamini wa mafunzo hayo yamegharimu kiasi
cha Dola za Kimarekani 20,000 kupeleka kwenye mradi wake wa elimu ya usalama
barabarani.
Tatal imekuwa
ikidhamini mafunzo ya Usalama barabarani kila mwaka kutokana na
kutenga bajeti hiyo kwa ajili ya
mafunzo hayo.
Utengaji huo wanatumia Boksi la
Usalama barabrani ambao ni mradi wa kuendelea kwa kipindi cha miaka 10 na utakuwa
ukitolewa nchi nzima, kwa maeneo yenye kiwango kikubwa cha hatari za ajali kwa
wanafunzi.
Mpaka sasa zaidi ya wanafunzi 150,000
wamefundishwa juu ya usalama barabarani katika jiji la Dar es Salaam, Kibaha na
Bagamoyo.
Boksi la usalama barabarani lina alama za
barabarani, maelekezo ya elimu ya usalama barabarani kwa mwanafunzi, maelekezo
ya usalama barabarani kwa mwalimu, mfano wa barabara yenye alama na vifaa
vingine kama viakisi mwanga, vyeti pamoja na kalamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...