Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
KIKOSI cha Usalama Barabarani kimeanzisha mbinu mpya za ulipaji wa makosa ya barabarani kwa njia ya Mtandao kupitia kampuni ya Max Malipo pamoja na baadhi ya benki.
Kuazishwa kwa mashine hizo imetokana na kuwepo kwa malalamiko ya madereva juu ya kupata risti ambazo si halali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP,Mohamed Mpinga amesema kuwa kwa kuanzia majaribio kwa Mkoa wa Dar es Salaam wataanza na mashine 300 pamoja na kamera 12.
Kamanda Mpinga amesema zoezi hilo linaanza kesho kwa kuingiza mashine 150 na baaada ya majaribio wataingia katika mikoa mingine.
Amesema gari ikiwa na kosa inaingizwa katika mfumo hivyo watu wanatakiwa kulipa kutokana na kosa kuchelewa zaidi ya siku saba za faini itatozwa kwa asilimia 25 baada ya siku 14 asilimia 50 kushindwa kabisha mtu atafunguliwa mashitaka ya kifungo cha miezi miwili au faini pamoja na kufungia leseni kwa miezi sita.
Mashine za kutolea risti pamoja na kamaera 12 zimetolewa na Kampuni ya Max Malipo ili kuweza kushirikiana na jeshi la polisi katika kudhibiti fedha zinazolipwa.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Max Malipo, Bw. Ahmed Lussasi amesema kuwa wameangalia mazingira yote katika uendeshaji wa mashine hizo katika ulipaji makosa ya usalama barabarani.
Lussassi amesema kuwa wataendelea kushirikiana kutokana na kutoa huduma kwa muda mrefu na kuwa na mafanikio.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani, DCP Mohamed Mpinga akizungumza na waandishi wa habari juu ya ulipaji wa makosa ya barabarani kwa njia kieletroniki iliyofanyika leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP,Mohamed Mpinga akionyesha mfano wa risti iliyotoka katika mashine baada ya ulipaji wa kosa la usalama barabarani leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Max Malipo,Ahmed Lussasi akizungumza na waandishi juu walivyojipanga katika kutoa huduma ya usalama barabarani ,leo jijini Dar es Salaam.kushoto 02.Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga
Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamanda Mpinga leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...