Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2015/2016 inatazamiwa kuanza kutimua vumbi jumamosi Septemba 12, 2015 kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti nchini.

Ndanda FC ya Mtwara watakua wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nagwanda Sijaona mjini Mtwara, Wana kimanumanu African Sports watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Wana Lizombe Majimaji wakiwa wenyeji wa maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Azam FC watakua wenyeji wa Tanzania Prisons kaika uwanja wa Chamazi Complex, Stand United FC chama la wana watawakaribisha Mtibwa Sugar katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto Africans watawakaribisha Mwadui FC uwanja wa CCM Kirumba na Mbeya City watacheza na Kagera Sugar katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Jumapili Ligi Kuu itaendelea kwa mchezo mmoja tu utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo mabingwa watetezi wa kombe hilo Yanga SC watawakribisha wagosi wa kaya Coastal Union.

Katika hatua nyingine klabu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera itatumia  Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kwa mechi zake za nyumbani dhidi ya Toto Africans (Sept 26), JKT Ruvu (Sept 30), Tanzania Prisons (Oct 4) na Yanga (Oct 31).

Mabadiliko hayo yamefanyika kupisha shughuli ya uwekaji nyasi bandia inayoendelea kwenye uwanja wao wa Kaitaba mjini Bukoba unaofanywa na wataalamu kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...