Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damiani Lubuva.

Na Anitha Jonas – MAELEZO.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi  nchini  imefuta rufaa 38 za wagombea nafasi za ubunge kati ya 54 zilizowasilishwa kupinga baadhi ya wagombea hao kwa kuwatuhumu kutotimiza vigezo mbalimbali na kusema wagombea hao wanaweza kuendelea na Kampeni majimboni mwao.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchaguzi  Bw.Kailima Ramadhan kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Alisema kuwa baada ya Wakurugenzi wanaoshughulikia uchaguzi kuzipitia ,waligundua kuwa rufaa hizo waliziona hazina mantiki na kukosa ushahidi wa kutosha.

“Wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa katika uchaguzi ni 16 na Tume imewarudisha wagombea 13 kati ya hao na waliobaki watatu ,Tume imeridhia maamuzi ya wasimamizi wa Uchaguzi”,alisema Bw.Ramadhani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...