Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye (Pichani) amewataka wagombea wa
vyama mbalimbali vya siasa kuacha kutumia Udini au Ukanda kutokana na kufanya hivyo ni
kuigawa nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam, Nnauye amesema kuwa kuna watu katika kampeni wamejitokeza
kutumia udini na ukanda vitu ambayo ni kinyume na maadili ya uchaguzi ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC).
Amesema kuwa baadhi ya wagombea
wameonekana katika ibada wakitaka wachaguliwe katika nafasi walizogombea hali
ambaya italeta mpasuko wa udini dhidi ya
watu wengine.
AIDHA Nape amesema kuwa kutokana maadili
yaliyotolewa na NEC wagombea wafuate katika kuendesha kampeni ambazo haziwagawi
watu.
“Uchaguzi huu watu wasitumie udini au
ukanda kwani unagwa watanzania hivyo kila mtu afanye kampeni za kistaarabu na
NEC ichukue hatua kwa watu wanaotumia udini”amesema Nape.
Ni wazi kwamba kila mtu afuate taratibu na kanuni zinazokubalika. Angalizo hili ni kwa vyama vyote, kunzia CCM. Nape Nnauye mwenyewe alifanya kosa aliposema kuwa CCM itashinda, hata kwa goli la mkono. Kwangu kama raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa, kauli ile ilikuwa inaashiria shari.
ReplyDeleteHakuna sababu ya kugawanya wananchi wa Tanzania.
ReplyDelete