Mwalimu wa masomo ya Sayansi wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Mbezi beach jijini Dar es Salaam, Elibariki John akiwaelekeza wanafunzi wa kidato cha pili, Jacqueline James(kushoto) na Ibrahim Juma  wa shule hiyo jinsi ya kutafuta  taarifa za maarifa ya masomo  ya sayansi kwa njia ya kompyuta mpakato zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation miezi mitatu iliyopita kupitia mradi wake wa kompyuta mashuleni unaoendeshwa na Learning In Sync.
Mariam Mwishaha na Khairat Massoud - wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Mbezi beach jijini Dar es Salaam wakimsikiliza kwa umakini Mwalimu wa masomo ya Sayansi wa shule hiyo,Elibariki John(kushoto) wakati akiwafundisha masomo hayo kupitia kompyuta mpakato walizopatiwa msaada na Vodacom Foundation miezi mitatu iliyopita kupitia mradi wake wa kompyuta mashuleni unaoendeshwa na Learning In Sync.
Wanafunzi wa kidato cha pili wa  shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Mbezi beach jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza mwalimu wao wa masomo ya Sayansi Elibariki John,akiwafundisha somo hilo kwa vitendo kupitia kompyuta mpakato zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation miezi mitatu iliyopita kupitia mradi wake wa kompyuta mashuleni unaoendeshwa na Learning In Sync.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Waswahili wanasema "Pokea hidaya japokuwa dhaifu" ni kweli usemi huo nikiuhusisha na hizo Kompyuta Mpakato, maana ukizitizama kwa ghafla moja tu, unaweza kudhania ni zile za 'toy' kumbe ni real thing. Kwa kweli hongereni sana 'Vodacom Foundation' pia nawapongeza sana na kuwashkuru kwa msaada huo ambao ni muhimu sana. At least wanafunzi wataweza kujifunza mengi ya manufaa na kuweza kupata ama kutafuta taarifa mbali mbali za maarifa ya masomo yao, khususan hayo ya Sayansi na masomo mengineyo mbali mbali na khasa tukizingatia generation ya sasa hivi ni ya 'Science and technology' hivyo kwa kiasi kikubwa zitawasaidia kupiga hatua zaidi kitaaluma. Pongezi za dhati kwa Vodacom Foundation naamini na wengine mithli yenu wataiga mfano wenu kwa manufaa na maendeleo ya kitaaluma kwa shule zetu nchini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...