Mwalimu
wa masomo ya Sayansi wa shule ya sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi
Mbezi beach jijini Dar es Salaam, Elibariki John akiwaelekeza wanafunzi
wa kidato cha pili, Jacqueline James(kushoto)
na Ibrahim Juma wa shule hiyo jinsi ya kutafuta taarifa za maarifa ya
masomo ya sayansi kwa njia ya kompyuta mpakato zilizotolewa msaada na
Vodacom Foundation miezi mitatu iliyopita kupitia mradi wake wa kompyuta
mashuleni unaoendeshwa na Learning In Sync.
Mariam
Mwishaha na Khairat Massoud - wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya
sekondari ya Mtakuja iliyopo Kunduchi Mbezi beach jijini Dar es Salaam
wakimsikiliza kwa umakini Mwalimu wa masomo
ya Sayansi wa shule hiyo,Elibariki John(kushoto) wakati akiwafundisha
masomo hayo kupitia kompyuta mpakato walizopatiwa msaada na Vodacom
Foundation miezi mitatu iliyopita kupitia mradi wake wa kompyuta
mashuleni unaoendeshwa na Learning In Sync.
Wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari ya
Mtakuja iliyopo Kunduchi Mbezi beach jijini Dar es Salaam,wakimsikiliza
mwalimu wao wa masomo ya Sayansi Elibariki John,akiwafundisha
somo hilo kwa vitendo kupitia kompyuta mpakato zilizotolewa msaada na
Vodacom Foundation miezi mitatu iliyopita kupitia mradi wake wa kompyuta
mashuleni unaoendeshwa na Learning In Sync.
Waswahili wanasema "Pokea hidaya japokuwa dhaifu" ni kweli usemi huo nikiuhusisha na hizo Kompyuta Mpakato, maana ukizitizama kwa ghafla moja tu, unaweza kudhania ni zile za 'toy' kumbe ni real thing. Kwa kweli hongereni sana 'Vodacom Foundation' pia nawapongeza sana na kuwashkuru kwa msaada huo ambao ni muhimu sana. At least wanafunzi wataweza kujifunza mengi ya manufaa na kuweza kupata ama kutafuta taarifa mbali mbali za maarifa ya masomo yao, khususan hayo ya Sayansi na masomo mengineyo mbali mbali na khasa tukizingatia generation ya sasa hivi ni ya 'Science and technology' hivyo kwa kiasi kikubwa zitawasaidia kupiga hatua zaidi kitaaluma. Pongezi za dhati kwa Vodacom Foundation naamini na wengine mithli yenu wataiga mfano wenu kwa manufaa na maendeleo ya kitaaluma kwa shule zetu nchini.
ReplyDelete