Zaidi ya wanafunzi laki saba 7.7 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza darasa la saba katika vituo zaidi ya elfu 16 nchni nzima kuanzia Septemba 9 hadi 10 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Daktari Charless Msonde amesema kati ya wanafunzi
hao wavulana laki tatu na sitini na moja elfu sawa na asilimia 45.6, wasichana ni
laki nne na kumi na nne elfu sawa na asilimia 53.4, ambapo masomo
yatakayotahiniwa ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na maarifa
ya jamii.
Amezitaka kamati za mitihani za mikoa na wilaya kuhakikisha
taratibu za mitihani zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vituo
vya mitihani vinakuwa salama, hususani katika kipindi hiki ambacho
baadhi ya viwanja vya shule za msingi vinatumiwa na vyama vya siasa kwa
ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu.
Ni kuwatakia wanafunzi wa darasa la saba kote nchini mtihani wa mafanikio.
ReplyDeleteYaani nchi nzima ni wanafunzi laki 7 tu?
ReplyDeletemaisha safari ndefu jamani...dogo ndio wanatupa karata zao.. all the best!
ReplyDelete