Wakulima wakifurahia mbegu bora za mahindi, alizeti pamoja na mbolea mara baada ya kukabidhiwa na meneja miradi wa kampuni ya Agrics. Wakulima walionufaika na mbegu hizo ni pamoja na Maswa, Meatu na Shinyanga vijijini.
Afisa Miradi wa kampuni ya Agrics Ltd, Bwana Semeni Kime (wa pili kulia) akifurahi na wakulima wa kijiji cha Mwakabeya baada ya kuwakabidhi wakulima hao mbegu za mahindi, alizeti pamoja na mbolea kwa ajili ya msimu mpya kilimo.
Kampuni ya Agrics imetimiza ahadi ya kuwakabidhi mbegu bora za mahindi, alizeti na mbolea wakulima wa Maswa, Meatu na Shinyanga vijijini. Zoezi hili limefanyika kwa wakati kufuatia msimu mpya wa kilimo kutazamiwa kuanza hivi karibuni. Kampuni ya Agrics iliwapa fursa wakulima kuchagua aina ya mbegu wazitakazo ili kuhakikisha wanapata kile wakipendacho. Wakulima wanaendelea kuandaa mashamba yao huku wakiwa huru kabisa kwani tayari Agrics imewapatia mbegu zao kwa mkopo nafuu kabisa na wametanguliza asilimia 25%. Zoezi la kukabidhi mbegu lilisindikizwa na viongozi mbalimbali wa vijiji ili kuhakikisha wakulima wanajipatia mbegu zao kwa manufaa ya kijiji na mkoa kwa ujumla.
Kusoma zaidi bofya HAPA.
Kusoma zaidi bofya HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...