Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akizungumza kabla ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’ lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akikata utepe kama ishara ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’, lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Kumbu Kumbu iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Priscilla Moshi (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Shule, Mwemba Mwilima (wa tatu kushoto), Wafanyakazi wa Airtel na watoto wa chekechea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kumbukumbu, Priscilla Moshi (kushoto) na Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya (wa pili kulia), wakiwa na watoto wa Chekechea, baada ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’, lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi wa Airtel kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika shule hiyo iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Airtel wakifurahi na watoto wa Chekechea katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, baada ya kukabidhi darasa la awali ‘Chekechea’, lililokarabatiwa kwa hisani ya Wafanyakazi hao, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika shule hiyo iliyopo Block 41, jijini Dar es Salaam jana.
KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kampeni yao ya “Airtel Tunakujali” inayoendeshwa na wafanyakazi wake imekabidhi darasa kwa shule ya msingi kumbukumbu Jijini Dar es Salaam ambalo imelikarabati kwa ajili ya wanafunzi wa awali maarufu kama chekechea.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alielezea umuhimu wa ukarabati wa darasa la chekechea kwa wafanyakazi wa Airtel.
Leo Airtel, kupitia mpango wetu wa “Airtel Tunakujali", tunatimiza dhamira yetu tuliyotoa ya kuwezesha shule ya msingi Kumbukumbu kuwa na uhakika na mazingira salama ya kusomea kwa wanafunzi wawapo hapa shuleni.
Kwani elimu bora huanzia kwenye hatua ya awali hivyo ukarabati wa darasa hili utakuza chachu ya wanafunzi hawa wadogo kujijengea mazingira ya kupenda kusoma wakiwa wakubwa”.
Akifafanua amesema, “wanafunzi wanapokuwa shuleni walimu huwa watu muhimu sana kwao, kwani huwafundisha watoto misingi bora ya kuishi hapa duniani, ambapo uwepo wa mazingira mazuri ya kufundishia huwapa morali walimu.
Ushirikiano wetu na shule ya msingi Kumbukumbu hautaishia hapa kwani tumepanga kuiwezesha ili iwe shule bora ndani ya manispaa ya Kinondoni na taifa kwa ujumla” aliongeza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...