Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimnowa bondia Lulu Kayage wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake wa kugombania mkanda wa taifa desemba 25 na bondia Mwanne Haji mpambano utakaofanyika mkoa wa Morogoro katika uwanja wa jamuhuri picha na SUPER D BOXING NEWS
BONDIA LULU KAYAGE
Bondia Lulu Kayage kushoto akielekezwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D'  jinsi ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini 'upcut' ambazo zinapigwa mbavuni Kayage anajiandaa na mipambano yake mbalimbali ya kitaifa na ya kimataifa picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimnowa bondia Lulu Kayage wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake wa kugombania mkanda wa taifa desemba 25 na bondia Mwanne Haji mpambano utakaofanyika mkoa wa Morogoro katika uwanja wa jamuhuri picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

BONDIA wa kike Lulu Kayage ameingia kambini kwa ajili ya mapambano yake ya kimataifa na kitaifa yatakayo mkabili siku za usoni bondia huyo ambaye ana uchu wa kufika mbali katika mchezo wa masumbwi nchini

ambapo Desemba 25 ata pambana na bondia Mwanne Haji kugombania ubingwa wa taifa katika mpambano wa raundi kumi utakao fanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro


bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' uku kocha na mshauli wa karibu wa bondia huyo akiwa ni Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anaratibu mapambano mbalimbali ya bondia huyo ndani na nje ya nchi.
Kayage ametamba kumsambalatisha mwanne Haji kama alivyo mfanya mkaburu wakati wa mpambano wake uliofanyika agost 9 uko afrika ya kusini na kuendeleza ubabe wake.
na kocha Rajabu Mhamila 'Super D' aliongeza kwa kusema Lulu ana moyo wa mazoezi na anajituma hivyo watanzania watambue wamepata mwokozi atakaeleta furaha katika mioyo yao na kuipeperusha vema bendera ya taifa nchini kwa kuwa nia anayo uwezo anawo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naona huyu Super D ni mtu mwenye moyo sana kusaidia maendeleo ya mchezo wa ngumi. Je, kuna uwezekano wa wafadhili kusaidia jitihada zake? Mfano kumpatia eneo na vifaa kwa harakati zake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...