Meneja wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kumpata mshindi wa shindano la kubuni maneno ya Kanga kupitia kipindi cha UHONDO ambacho huruka hewani kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa alasiri, kikiwa na Matangazaji mahiri Dina Marios, kikao hicho kimefanika leo jijini Dar es Salaam, katikati ni mshindi wa shindano hilo Sekela Richard na wakulia ni Matangazaji wa Efm Radio Dina Marios.
Matangazaji mahiri Dina Marios, akimkabidhi kitita cha shilingi Kitanzania milioni moja. mshindi wa shindano hilo, Sekela Richard kulia ni Meneja wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo
Picha na Emmanue Massaka.
MENEJA wa Mawasiliano Efm, Denis Ssebo shindano hilo halitaishia hapo, kwani baada ya kupata mshindi neno lake la Ushindi zitatengenezwa kanga zitakazoandikwa neno hilo ikiwa ni hatua ya pili sasa ya kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi.
Zikishatengenezwa kanga hizo, Efm kupitia kipindi hicho cha Uhondo, itatatoa nafasi kwa wanawake kutengeneza pesa na kujikwamua kwa kuuza Kanga hizo na Mwanamke yoyote hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani atachukua kanga hizo na kuziuza ambapo kwa kila doti moja ya kanga atapata asilimia 30% ya pesa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...