TIMU ya taifa ya mpira wa magongo ya wanawake kesho inacheza mechi yake ya kwanza ya ufunguzi dhidi ya
zimbambwe itakayopigwa nchini Afrika kusini,katika mashindano kuwania kufuzu michuano ya Olympic ya mwaka 2016 ambayo itafanyika mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil.
Kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya mpira wa Magongo Varentina Quaranta amesema kwa upande wa wanaume mechi yao ya ufunguzi watacheza na misri siku ya jumapili.
Kocha Quaranta ambaye yuko na timu nchini afrika kusini amesema wachezaji wote wako tayari na morali ya kutosha kuelekea katika mashindano hayo,huku pia akitoa shukrani kwa benki ya NMB na baadhi ya wadau wa mchezo huo kwa kuwezesha safari hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...