Maendeleo makubwa yamepatikana katika kupunguza kuenea kwa VVU.
Hata hivyo, ambukizo moja katika kila maambukizo kumi mapya huwapata watoto wanaozaliwa japokuwa asilimia 90 ya maambikizi haya yangeweza kuzuilika. Wasichana pia wamo hatarini zaidi kuambukizwa VVU kuliko wavulana. Kila ambukizo jipya la kijana aliye chini ya miaka ishirini linadhihirisha kushindwa kuwapatia vijana elimu ya afya ya uzazi, taarifa, stadi na huduma zitakazowawezesha kujilinda. Unyanyapaa na ubaguzi vinaendelea kudhoofisha uwezekano wa wanawake kupata huduma.
Fanya kazi pamoja na washiriki wote katika kupanua huduma na matibabu yatakayoangamiza kabisa maambukizi ya VVU ya mama kwa mtoto ifikapo mwaka 2015. Hakikisha kuwa watoto wote wenye VVU na UKIMWI wanapata matibabu wanayoyahitaji.
Toa ahadi ya kuongeza rasilimali katika kuwakinga vijana, hasa wasichana dhidi ya VVU na UKIMWI kwa kuunga mkono mpango wa kitaifa wa kuzuia VVU.
Saidia katika kuanzisha huduma za afya zinazowalenga vijana na mipango madhubuti ya stadi za maisha ambazo zitawapa taarifa na kuwawezesha, hasa wasichana kupunguza uwezekano wao wa kuambukizwa VVU na UKIMWI.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...