Meneja wa Wateja Binafsi wa First National Bank, Francois Botha na Meneja wa Usambazaji na Matawi wa benki hiyo wakizindua mpango maalum unaohamasisha Watanzania kujiwekea akiba na kujiwekea mustakabali salama kifedha. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam leo Oktoba 1, 2015.

BENKI ya FNB Tanzania imetoa wito kwa Watanzania kujijengea mustakabali salama kifedha kwa kuendelea kuweka akiba zaidi benki kupitia fursa ya mpango mpya wa benki hiyo wa “Weka akiba na ushinde”.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha wakati akizindua mpango huo jijini Dar es salaam ambapo alisistiza umuhimu wa kuweka akiba. Mpango huo wa Weka Akiba na Ushinde utaanza tarehe 1 Oktoba na kuendelea mpaka mwisho wa Disemba 2015.

Ikiwa ni sehemu ya mpango huo utakaodumu kwa miezi mitatu, wateja waliopo na wateja wapya wataingizwa moja kwa kwenye droo kutokana na akiba ya kila shilingi 50,000 watakayoweka kwenye akaunti zao, kwahiyo watakaoweka akiba zaidi watapata nafasi ya kushinda shilingi milioni 5 ambazo zitatolewa kila mwezi kwa kipindi chote cha kampeni hiyo ambayo iko wazi kwa watu wote kushiriki.

Botha alisema, “Katika kuendeleza utamaduni wa benki hii kuwatunuku na kuwanufaisha wateja wake huku ikiendelea kutoa huduma za kisasa za kibenki, FNB inatoa fursa hii kwa wateja kuweza kujinufaisha kutokana na kuweka akiba huku wakijijengea mustakabali salama kifedha”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...