Afisa Masoko wa Kampuni ya Global Education Link (GEL) wa Tawi la Arusha, Regina Lema akitoa maelezo kwa mmoja ya wageni waliofika katika maonyesho yaliyoandaliwa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) yanayofanyika jijini Arusha sambamba na kongamano la saba la elimu ya juu lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015.
Chuo Kikuu cha Muhimbili cha jijini Dar es Salaam kimeshiriki katika maonyesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) yanayofanyika jijini Arusha sambamba na kongamano la saba la elimu lililoanza leo Oktoba 1 -2, 2015.
Mmoja ya washiriki ambaye amebuni mtambo wa kuchuja maji akitoa maelezo machache.
Mwakilishi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Memorial, akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ambaye aliambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya.
Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Mandela cha jijini Arusha, akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi Profesa Awadh Mawenya, Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania aliyeambatana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya. Picha zaidi BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. UDSM kimeshakuwa chuo kidogo.

    ReplyDelete
  2. Nicha 10 kati ya vyuo bora barani Afrika; cha kwanza Afrika mashariki na kati.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...