Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa Ijumaa, Oktoba 23, 2015, amewateua Makatibu Wakuu wanne wapya wa wizara
mbali mbali.
Aidha,
Rais Kikwete amewateua Naibu Makatibu Wakuu wapya watano, amewateua Makatibu
Tawala wa Mikoa wawili na pia amewahamisha Naibu Makatibu Wakuu wawili.
Kwa
mujibu wa uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Ndugu Hab Mkwizu kuwa Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Profesa Elisante Ole Gabriel
kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo; Dkt.
Yamungu Kayandabila kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia na Mhandisi Omari Chambo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini.
Aidha,
kwa mujibu uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua Mhandisi Paul M. Masanja kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati
na Madini; Dkt. Maria Mashingo kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na
Uvuvi na Ndugu Zidikheri M. Mundeme kuwa
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Wengine
walioteuliwa kuwa Naibu Makatibu Wakuu ni Ndugu Tixon T. Nzunda ambaye anakuwa
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Ndugu
Emmanuel Kalobelo ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia.
Walioteuliwa
kuwa Makatibu Tawala wa Mikoa ni Ndugu Eliakim Maswi ambaye anakuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Manyara na Mhandisi Madeni Kipande ambaye anakuwa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katibu Mkuu ambaye anahamishwa ni Bibi Sihaba Nkinga
ambaye anakwenda kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Wanawake, Jinsia na
Watoto kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Naibu
Makatibu Wakuu wanaohamishwa ni Ndugu John T. Mngodo ambaye anahamishiwa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutoka Wizara ya Uchukuzi na Ndugu Mwamini Juma Malemi ambaye anakwenda
kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Wateuliwa
hao wote wataapishwa asubuhi ya leo, Jumamosi, Oktoba 24, 2015, Ikulu mjini
Dar es Salaam.
Jamaa wamepiga bao dakika za majeruhi, Hongereni
ReplyDeleteOle Gunnar Solskjær
ReplyDelete