Na Sultani Kipingo

RAIS  Jakaya Mrisho Kikwete leo amekabidhi magari 399 mapya kwa ajili ya kufanyia kazi kwa Jeshi la Polisi Tanzania katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Mafunzo ya Polisi kilichopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es  Salaam. 

Makabidhiano hayo yalifanyika mbele ya  Waziri wa Mambo ya ndani  Mhe Mathias Chikawe Inspekta  Jenerali wa Polisi  IGP Ernest Mangu na maofisa mbalimbali wa jeshi hilo.
IGP Mangu Alisema magari hayo 20 ni ya kutema maji ya kuwasha  na mengine ya kawaida kwa ajili ya matumizi ya kufanya doria na shughuli zingine za jeshi la polisi. 
Rais Kikwete alisema kutokana na kukabidhi gari hizo wapo ambao watasema kwamba zimekuja kwa ajili ya uchaguzi jambo ambalo amelikanusha vikali pia amemtaka IGP Mangu asiogope  maneno ya watu kwani kusema ni kawaida yao.
"Jambo la kushukuru ni kwamba kampeni za mwaka huu kila mgombea amekua akipanda jukwaani na kutoa ahadi zao kwa amani na usalama hii yote ni kutokana na kazi nzuri ya jeshi la Polisi.  


"Hivyo endeleeni kufanya kazi kwa weledi katika kipindi hiki  cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili ijayo" alisema Kikwete.

Aliongeza kwa kusema kwamba anafurahi kumaliza muda wake madarakani huku akiwa ametimiza ahadi ya kuwapatia  magari Jeshi la Polisi ili kuongeza ufanisi wao. Magari yaliyobaki yanatarajiwa kuingia nchini  kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Akizungumza   katika hafla  hiyo IGP  Mangu amemshukuru Rais Kikwete  kwa kutimiza ahadi  ya kuwapatia magari ambayo yatawawezesha  katika kufanya kazi kisasa.

Akitoa salamu za Shukrani kwa kuhudhuria hafla hiyo Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Afande Abdulrahman Kaniki alimhakikishia Rais Kikwete kwamba magari hayo yatatumika ipaswavyo na kutunzwa vyema.
Afande Kaniki alisema kwamba Jeshi la Polisi daima litakuwa likihubiri na kutekeleza kauli mbiu yake ya kuwataka wananchi kuzingatia sheria pasina shuruti, na kusema kuwa kwa jeshi hilo limejiandaa kupambana na wachache wenye kutotii sheria bila woga.
"Lakini pale ambapo wachache wanataka kutulazimisha tutumie shuruti tutafanya hivyo na hatutakuwa na ajizi kwa sababu hilo ndilo jukumu letu tulilopewa kisheria na tutahakikisha kwamba sheria itachukua mkondo wake.

Mhe Rais nikuhakikishie kwamba hatutamuonea  mtu lakini pia hatutampendelea  mtu kwa nafasi yake yoyote aliyonayo. Sisi tutahakikishwa kwamba sheria inachukua mkondo wake na nchi inaendelea kuwa na amani na kuwa kisiwa cha amani kama ambavyo nchi za jirani zinakimbilia nchi yetu, hilo nikuhakikishie Mhe. Rais" alisema Afande Kaniki.

  Rais Kikwete akihutubia katika  Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
  Rais Kikwete akikata utepe katika  Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akimkabidhi IGP Mangu funguo za magari hayo  katika  Chuo Kikuu cha Mafunzo ya Polisi Kurasini jijini Dar es salaam leo Oktoba 20, 2015 katika sherehe ya  kukabidhi magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi.
 Rais Kikwete akikagua sehemu ya  magari 399 kati ya 777 yanayoletwa kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi wa  jeshi la polisi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Piga kura nenda nyumbani. Message sent loud and clear:)

    ReplyDelete
  2. Yaani magari hayaletwi kukabili jinai za kila siku. Jinai ihusuyo uchaguzi ndo inayojaliwa zaidi. Ama kweli uchaguzi ni haki kuu ya mwananchi na siyo afya, elimu, wala usalama. Mtakoma uchaguzi huu.

    ReplyDelete
  3. Fanya fujo uone cha mtema kuni, hakuna nafasi ya lutoana ngeu au kuvunja amani kwa sababu ya uchaguzi. Hiki ni kipindi acha lipite kwa amani tuendelee na maisha yetu.

    ReplyDelete
  4. Watu wasiotii sheria watatandikwa

    ReplyDelete
  5. Duh Kina ras makunja wamepata mzigo mpya ! Kazi TU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...