Ndugu Ray Power, ambaye amewahi kuwa Kocha wa Chama
Cha Soka na mkuu wa kitengo cha mpira wa miguu katika chuo kiitwacho Central
College Nottingham; ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi katika Kituo cha
Vijana cha Michezo kilichopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam (pichani).
Katika nafasi yake mpya, Ndugu
Power atasimamia mafunzo na Uongozi wa kituo kipya ambacho kinategemewa
kufunguliwa tarehe 19 ya Mwezi huu. Ndugu Power anachukua nafasi iliyoachwa
wazi na aliyekuwa Mkurugenzi wa kituo; Stewart Hall aliyejiunga na timu ya Azam
kwa mara nyingine kama Kocha Mkuu.
“ Hii ni
changamoto kubwa kwangu na ninaichukua kwa moyo mkunjufu. Kuna kiwango kikubwa
cha elimu kinachoendana bega kwa bega na michezo na sina shaka uzoefu wangu
kama kocha na kama muelimishaji ayehitimu mafunzo yake; vyote kwa pamoja
vitanipa uwezo unaotakiwa kwenye nafasi hii” alinena Ndugu Power ambaye ni
kocha mwenye leseni ya kiwango cha daraja la ‘A’ inayotolewa na Shirikisho la
Soka la Ulaya ( UEFA) na mwandishi maarufu wa ukuzaji wa soka la vijana.
Kituo cha Kijamii cha Michezo kitatoa uwanja wa
nyasi bandia ulio na ukubwa wa 3G, pamoja na viwanja viwili vinavyoruhusu
wachezaji watano watano kila upande, kiwanja kimoja chenye mchanga pamoja na
viwanja viwili vya mpira wa kikapu n.k
Ndugu Power aliongeza “ Filosofia yangu
itakuwa kwa mtu mmoja mmoja katika kituo, kumsaidia kila mmoja kuendelea; maana
kila mtu ana uwezo wake na udhaifu wake tofauti na mtu mwingine. Nimedhamiria
kusaidia ukuaji wa fursa za michezo na njia maalumu za kimpira wa miguu
zitakazo wawezesha vijana wa kitanzania kujiandaa kwa changamoto watakazo kabiliana
nazo siku za usoni”
Kituo cha vijana ambacho kimefadhiliwa na Symbion
Power, kitapata msaada wa kiufundi na mazoezi kutoka kwa Timu iitwayo
Sunderland AFC ambayo inashiriki ligi Kuu ya
Barclays ya Uingereza. Hii itakuwa ya kwanza ya namna yake ya kipekee
kwa hapa nchini Tanzania. Maelfu ya vijana wa kitanzania watafaidika na
muunganiko wa michezo, elimu na Ushiriki katika Shughuli za kijamii kwa kutumia
maarifa na utaalamu wa wakufunzi kutoka timu ya mpira ya Sunderland.
Paul Hinks, Mtendaji Mkuu wa Symbion Power alinena:
“ Kituo cha Vijana Jakaya Mrisho Kikwete ni kiungo cha kati cha Ushirikiano wa
kipekee kati ya Symbion Power, Timu ya mpira ya Sunderland na Tanzania na
tunaamini ubora alionao Bwana Ray pamoja na uzoefu wa timu ya mpira ya Sunderland
utatuwezesha kushuhudia ukurasa mpya wa maendeleo ya michezo nchini Tanzania
ni kizuri sana ila kipo mjini sana vijana wetu hawataconcentrate vizuri...kingefaa kupelekwa mkoani au nje ya mji panapo utulivu..vitakavyojengwa vipelekwa nje ya mji
ReplyDelete