Viongozi wa vyama vya siasa vitano AFP, UMD, CHAHUSTA, JAHAZI ASILIA NA DEMOKRASIA MAKINI kwa pamoja tumeungana kutoa wito kwa wanasiasa wenzetu, viongozi wa dini na wananchi wote kwa jumla kuhusiana na uchaguzi huu unaotarajiwa kufanyika ifikapo tarehe 25/10/2015 Tamko hili ni pamoja na:-
1. Tunawapongeza wagombea wote wa nafasi ya Urais kwa kuendelea kufanya kampeni kwa njia ya amani na Utulivu.
2. Tunawataka watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura wajitokeze kwa wingi siku ya tarehe 25/10/2015 kupiga kura kwa kuchagua viongozi wanaowataka kwa amani na Utulivu.
3. Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali, Urais, Ubunge na Madiwani waache kutoa maneno ya kuwatia hofu wapiga kura kwamba tunaweza kuibiwa kura na badala yake tuwahamasishe zaidi kujitokeza kwa wingii kupiga kura na kuiamini tume ya taifa ya uchaguzi kuwa watatenda haki kwa wagombea wote bila kujali hadhi ya chama cha siasa anachotoka mgombea. 4.Viongozi wa dini wanaotaka kuwafanyia kampeni wagombea wasifanye hivyo katika nyumba za ibaada na badala yake wakipenda kufany ahivo watumie majukwaa ya kisia sa na sio madhabahu. 5.Viongozi wa vyama vya siasa waache kutoa vitisho kwa wapiga kura kwa kuwatia hofu ya kutabiri kuwepo kwa umwagikaji wa damu.
6. Viongo wa asasi za kiraia wasiendelee kufanya tafiti na kuwapa ailimia wagombea kiushabiki bila ya kufuata maadili na kanuni za kitafiti mabyo matokeo ya tafiti zao zimekuwa zikileta mtafaruku katika jamii kwa kueta za ama kumdhoofisha mmoja kati ya wagombea waliotajwa katika tafiti husika.
7. Mwisho tunawataka watanzania wote kuwa makini na kuyadharau matamko yote yenye nia ya kuwatia hofu na kuendelea kuipenda nchi yetu ya Aamini na Utulivu katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Taifa letu. Na vilevile viongozi wa dini waendelee kuliombea taifa letu libaki kuwa na utulivu wakati wote wa uwepo wetu katika nchi yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nimehuzunishwa na kuwepo kwa wanasiasa wasioamini sayansi. Yaani watu wasifanye chunguzi za kisayansi kwa sababu tu kuna watu wengi wasiojua sayansi? Wote mlipita sekondari lakini mwalimu wenu wa hesabu hakuwafundisha takwimu vizuri au nyie hamkumfata mwalimu wenu vizuri.

    Maoni yangu: ukweli kwamba vyama fulani havifanyi vizuri isiwe sababu ya kukatazwa wanahabari na wanasayansi wanoelimisha jamii kwa kutumia habari na data kufanya kazi zao. Wananchi wazoee hilo ndo tutaenda mbele na siyo kuzuia ili wananchi waendelee kuwa walivyo huko nyuma.

    Mabadiliko hudumu kwenye jamii yeyote iliyo nyuma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...