Na Dotto Kahindi

Kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia uendeshaji wa baiskeli katika nchi mbalimbali Barani Afrika imeingia Tanzania Octoba 17 kwa waendesha baiskeli 21 kutoka Tanzania kuwapokea wenzao kutoka Malawi.

Kampeni hiyo ambayo imeanzia Msumbiji, Afrika Kusini, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi na hatimaye Tanzania na itatia nanga Kenya mapema mwezi novemba mwaka huu.

Msafara huo wa waendesha baiskeli kwa Tanzania umeanzia kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu ambapo unataratia kwenda mpaka Namanga watakapoukabidhi kwa waendesha baiskeli wa Kenya.

Kwa mujibu wa Meneja Miradi wa shirika la Norwegian Church Aid, Augustina Mosha lengo la msafara huo ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa kutumia vijana kutoka kwenye taasisi za kidini nchini.

Anasema msafara huo utahusisha pia uchukuaji wa saini za wananchi ili kuweka imani zao kwa viongozi wa kiserikali ambao watakwenda kwenye mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP21 utakaofanyika Desemba mwaka huu huko Paris, Ufaransa.

Mama Mosha anasema kuwa wameamua kutumia uendeshaji wa baiskeli kama njia ya kuhamasisha jamii juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa sababu chombo hicho ni rafiki wa mazingira na hakichangii uzalishaji wa hewa ukaa.
Picha zote na tabianchi blog
Waendesha baiskeli kutoka Malawi wakiwasili kwenye mpaka wa Tanzania na nchi hiyo tayari kwa kukabidhi kijiti cha kampeni hiyo kwa wenzao wa Tanzania.
Mmoja wa waendesha baiskeli Tanzania ambaye pia ni Ofisa Miradi wa Norwegian Church Aid, Tanzania, Gilbert Mworia.
Meneja Miradi wa shirika la Norwegian Church Aid, Augustina Mosha akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabianchi kupitia uendeshaji wa baiskeli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...