KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI, DKT SHAABAN MWINJAKA AZINDUA BODI YA KAMPUNI YA MILIKI YA RASILIMALI ZA RELI (RAHCO), KWA NIABA YA WAZIRI WA UCHUKUZI, LEO ASUBUHI
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akitoa maelekezo kwa Niaba ya Waziri wa Uchukuzi, kwa Wakurugenzi wa Bodi ya Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), leo asubuhi wakati akizindua bodi hiyo katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (katikati) akikabidhi Sheria ya kuanzishwa kwa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO) kwa Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni hiyo Profesa Mwanuzi Fredrick (wa kwanza kulia), kwa Niaba ya Waziri wa Uchukuzi, leo asubuhi mara baada ya kuizindua katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi. Anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasimali za Reli (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Profesa Mwanuzi Fredrick akitoa neno la shukrani mara baada ya Uzinduzi wa Bodi ya Kampuni hiyo leo asubuhi katika ofisi za Wizara ya Uchukuzi.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (wa tatu kutoka kushoto mstari wa kwanza) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Bodi ya Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli( RAHCO), na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, mara baada ya uzinduzi wa bodi hiyo leo asubuhi.

(Habari PIcha na Kitengo cha MAwasiliano Serikalini-Uchukuzi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...