Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la Fasjet kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Jimmy Kibati amesema kampuni yao imefikia makubaliano na TFF ya kuwa msafirishaji rasmi wa timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi 2018 dhidi ya Algeria.
Jimmy amesema katika safari hiyo, Fastjet itatoa ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 156 walioketi, sambamba na wafanyakazi wa ndenge, ambapo wao wametoa punguzo la asilimia 35 katika gharama nzima ya safari ya kuelekea Algeria.
Aidha Jimmy ameongeza kuwa safari hiyo itakua ni ya masaa 7 ambapo ndege ikitoka Dar es salaam itatua Djamena – Chad kuongeza mafuta kabla ya kuendelea tena na safari mpaka nchini Algeria.
Naye katibu wa kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda aliwashukuru Fastjet kwa kukubali kuwa wasafirishaji rasmi wa TaifA Stars kwa mechi dhidi ya Algeria, huku akisema gharama za safari za mtu mmoja kusafiri ni dolla 800 kwenda na kurudi.
Teddy amewaomba watanzania, wapenzi, washabiki wa mpira wa miguu wanaotaka kusafiri kufika ofisi za TFF zilizopo Karume kwa ajili ya kujiandiksha na kuelekea taratibu nzima za safari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. INAPITIA NDJAMENA CHAD HUKO KUNA ISIL, AL QAEDA WANAOTUNGUA NDEGE ZA ABIRIA NA ZA KIVITA. KWA NINI MSIPITIE LAGOS AU ACCRA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...