JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi inapenda kuwataarifu Wananchi
wote kwamba kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba ni Siku ya Makazi Duniani ambayo huadhimishwa Duniani kote.
Nchini, mwaka huu tarehe 05/10/2015 – Jumatatu,
Maadhimisho ya siku hii yanategemewa kufanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa mbili na nusu asubuhi (2:30) mpaka saa nane mchana (8:00).
Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni;
“Maeneo
ya Umma kwa Wote”
Mgeni rasmi katika Maadhimisho haya anatarajiwa
kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe.William Lukuvi.
“Wananchi
wote mnakaribishwa”
Imetolewa na Katibu
Mkuu
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Tuhamasishe uboreshaji wa makazi ya kila mtanzania kwa manufaa yetu wenyewe na afya zetu.
ReplyDelete