JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
 TAARIFA KWA UMMA
 Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inapenda kuwataarifu  Wananchi wote kwamba kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba ni Siku ya Makazi Duniani  ambayo huadhimishwa Duniani kote.

Nchini, mwaka huu tarehe 05/10/2015  –  Jumatatu, Maadhimisho ya siku hii yanategemewa kufanyika katika viwanja vya Karimjee kuanzia saa mbili na nusu asubuhi (2:30) mpaka saa nane mchana (8:00).

Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni; 
“Maeneo ya Umma kwa Wote”

Mgeni rasmi katika Maadhimisho haya anatarajiwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe.William Lukuvi.

“Wananchi wote mnakaribishwa”

Imetolewa na Katibu Mkuu

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tuhamasishe uboreshaji wa makazi ya kila mtanzania kwa manufaa yetu wenyewe na afya zetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...