Lulu Ally Mlupilo
19/10/2013 – 19/10/2015
Leo imetimia miaka miwili tangu utuache na kutuachia majonzi makubwa, ni mtihani mkubwa sana kwetu, umetuacha wapweke, lakini yote ni mipango ya Mwenyeezi Mungu, kwa kuwa ndiye Mpangaji wa kila kitu. Miaka miwili ni muda mrefu, lakini kwetu ni kama jana.
Kimwili haupo nasi, lakini kiroho daima tupo na wewe, tunakukumbuka na kukuombea kila siku, mapenzi yetu kwako yapo palepale. Unakumbukwa sana na Baba yako Ally Mlupilo, Mama yako Zainab Bakary Orty, watoto zako wapenzi, Hanimu, Tamimu na Iqra, Kaka yako Orty Ally, ndugu, jamaa na marafiki zako wote.
Mwenyeezi Mungu Ailaze roho yako mahala pema peponi, Akusamehe makosa yako na Akuweke kwenye pepo ya firdaus - Amina!
Mwenyeezi Mungu Akuweke mahala pema peponi, Ameen!
ReplyDeleteInna Lillahi Wainna Ilayhi Rajiun. Wenyeez Mungu akughufirie kwa yote, akunusurishe na adhabuze zote, akupumzishe katika kivuli chake na kesho In Sha Allah, Yaumul-Hisabu akujaaliye uwe ni miongoni mwa waja wake wema atakaowajaaliya kuingia katika pepo yake ya 'Jannatunnaeem' - AMEEN.
ReplyDeleteInna Lilahi Wa Inna Ilahi Rajiun, upumzike kwa amani, umetangulia sisi sote tupo nyuma yako. Mwenyeezi Mungu Akusamehe makosa yako yote, Amuweke mahala pema peponi, Ameen!
ReplyDelete