Gari ya ziada katika msafara wa Spika wa Bunge ikiwa imepinduka wakati wakiwa njiani kuelekea katika mazishi ya Marehemu Deo Filikunjombe huko Ludewa. Ajali hiyo imewahusisha Mlinzi wa Spika, Alphonse Mwakasege, Naibu Katibu wa Spika,Herman Berege na Mbunge wa Mafia anaemaliza muda wake, Mhe Abdulkarim Shah. Abiria wote wamepata majeraha madogo madogo na waliokolewa katika eneo hilo na Mhe. William Lukuvi, Mb na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi.
Picha kwa hisani ya Ofisi ya Bunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...