EAST AFRICAN COMMUNITY
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
KUNDI la waangalizi wa uchaguzi Mkuu nchini Tanzania
unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25, mwaka huu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanatarajia
kuwasili Dar es Salaam Jumapili, tarehe 18 October 2015 tayari kwa uangalizi wa uchaguzi kwa
upande wa Tanzania Bara na Visiwani.
Kuwasili kwa kundi la Jumuiya ya Afrika Mashariki
lenye takribani watu hamsini na tano, ni kuitikia mwaliko kutoka kwa Tume ya
Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kufuata Maazimio ya Baraza
la Mawazili la Jumuiya ya Afrika Mashariki juu ya uangalizi wa uchaguzi kwa
nchi Wanachama wa Jumuiya.
Kazi ya wasimamizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya
Afrika Mashariki itakuwa ni kuangalia kwa ujumla wake mazingira ya uchaguzi na
kutathmini kwa
kina mchakato wa uchaguzi nchini kote kabla, kipindi cha uchaguzi na baada ya
siku ya uchaguzi.
Kundi la waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya
Afrika Mashariki litaongozwa na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kenya, Mh. Awori Arthur Athansius Moody.
Kundi waangalizi
wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki litatangaza uwepowake inchini Tanzania
kwenye mkutano na Waandishi wa Habari utakaofanyika Jumatatu, tarehe 19,
October 2015, saa mbili na dakika thelathini (8.30am) asubui, New Africa Hotel,
Dar es Salaam.
·
NINI KITAFANYIKA- Kutoa taarifa ya kuwasili kwa
waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki
·
WAPI- New Africa Hotel, Dar es
Salaam
·
LINI- Tarehe 19th October 2015
from 8.30 am -10.30am
Ndugu Muandishi wa Habari, unaombwa kuthibitisha
uwepo wako kwenye mkutano huu kupitia anuani zifutazo hapa chini;
Owora Richard Othieno,
Press and Protocol Coordinator
EAC Election Observer Mission
New Africa Hotel
Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 784 835021;
Email: oothieno@eachq.org
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...