Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Kidato cha Nne Shule ya Sekondari Bwawani.
Wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Bwawani wakigani shairi lao mbele ya Mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil akimkabidhi cheti Mwanafunzi Mhitimu kwenye Mahafali ya Kumi na mbili ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Bwawani Oktoba 16, 2015(kulia kwa Mgeni rasmi) ni Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
Na Lucas Mboje, Pwani.
WAHITIMU wa kidato cha nne nchini wameaswa kuachana na fikria potofu kuwa elimu wanayoipata itawapatia ajira Serikalini au kwenye Sekta binafsi badala yake watumie elimu hiyo kama nyenzo muhimu ya kuwawezesha kujiajiri wao wenyewe.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Bw. Mbarak Abdulwakil alipokuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya kumi na mbili ya kidato cha nne katika shule ya Bwawani Sekondari iliyopo Mkoani Pwani.
"Katika hali ya sasa ya utandawazi yapo mambo kadhaa ambayo mtu binafsi anaweza kuyafanya na kujipatia kipato cha kujiendeleza maisha yake". Alisema Bw. Abdulwakil.
Bw. Abdulwakil amesisitiza kuwa wanachotakiwa kufanya wahitimu hao ni kuyasoma mazingira ya maisha popote watakapokuwa na kuamua namna ya kujiajiri ili mradi isiwe shughuli zinazopingana na sheria na maadili ya kijamii, kama vile kuuza madawa ya kulevya, ukahaba, unyang'anyi na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...