
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi
Na fredy mgunda,Ismani
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Ismani kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) William Lukuvi amembeza mgombea mwenzake anayegombea ubunge kwenye jimbo hilo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema Patrick Olle Sosopi na kusema kuwa Sosopi hata afanye hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Kauli ya Lukuvi aliitoa juzi wakati akiwahutubia wananchi wa vijiji vya Igingilanyi,Kising’a,Kinywang’ anga,Mkungugu,Matembo na Ilambilole vilivyopo tarafa ya Isimani katika Jimo la Ismani alisema kuwa Sosopi hawezi kuvaa viatu vyake kwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa maana hana staha ya kuweza kuwashawishi wananchi kuwaletea maendeleo na badala yake anawabeza wagombea wa chama cha mapinduzi CCM pamoja na mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa kusema kuwa kwa kipindi cha miaka 20 ya ubunge wa Lukuvi hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa na chama hicho.
“Mimi kiatu change navaa namba nane Sosopi anavaa namba moja hivi kweli ataweza kuwa mbunge wa jimbo hili?alihoji huku akishangiliwa sana na wananchi hao,kiukweli niwaambie kama mnataka maendeleo kichagueni CCM ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo na sio chama kingine.”alisema Lukuvi.
Kusoma zaidi bofya HAPA NA KUONA TIMU BAJAJ SIMIYU BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...