Dk.
Umanath Nayak, mshauri mkuu wa magonjwa ya saratani ya kichwa na shingo
pamoja na upasuaji kwa njia ya roboti katika hospitali ya saratani ya
Apollo Hyderabad nchini India.
Na Mwandishi Wetu,
SEKTA ya afya duniani imeshuhudia mapinduzi
yanayolenga kuongeza umri wa kuishi, ubora wa maisha, njia mbadala za uchunguzi,
njia bora za matibabu, na pia ufanisi na ubora katika huduma za afya.
Teknohama
imekuwa na mchango mkubwa sana katika maendeleo ya ndani ya sekta hii muhimu. Makampuni
yanayohusika na kutengeneza vifaa vya tiba hivi sasa yanalenga katika
kutengeneza roboti ambazo hufanya upasuaji kwa ufanisi zaidi bila madhara
makubwa kwa mgonjwa.
Kuna
matumaini sana katika upasuaji kwa kutumia teknolojia ya Roboti. Teknolojia hii
ni ishara ya mapinduzi katika sekta ya afya, na ni moja ya mambo muhimu
yanayoongelewa sana katika upasuaji hivi leo. Mfumo wa upasuaji kwa kutumia
roboti umeletwa ili kusaidia katika upasuaji mgumu, ambao hufanyika kwa shida,
au unaohusisha maeneo ambayo ni magumu kufikika na hatari. Kwa kutumia mikono maalumu
inayopatikana katika Roboti hilo upasuaji huo urahisishwa zaidi.
Mikono ya Roboti hudhibitiwa na kompyuta
inayoendeshwa na mpasuaji kwa kutumia mikono na miguu. Udhibiti huu ni sawa na ule
wa mchezo wa video, maarufu kama ‘video game’ ambao huwezesha upatikanaji kwa
usahihi zaidi wa maeneo magumu kufikika ikilinganishwa na njia iliyokuwa
ikitumika awali ya ‘laparoscopic’.
Kutumia matundu madogo sana, upasuaji wa aina hii unaweza kuondoa uvimbe
uliojificha pasipo uharibifu wa tishu na pia humsaidia mgonjwa kutokaa
hospitalini muda mrefu pamoja kupona ndani ya muda mfupi. Teknolojia hii
inapunguza hatari ya uharibifu wa mishipa na tishu katika eneo husika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...