Na Mwandishi wetu
Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imeshindwa kutamba mbele ya timu ya soka ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mechi maalum ya kuadhimisha miaka 16 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Bora, Kijitonyama, mabao ya NSSF yalifungwa na Linus  Bwegoge kwa shuti la nje ya eneo la hatari kutoka wingi ya kushoto na la pili lilifungwa kwa njia ya penati na Khalfan Waziri baada ya beki wa Taswa FC, Khatimu Nahela kumwangusha kwenye eneo la hatari msambuliaji wa NSSF, Ali Chuo.

Bao la Taswa lilifungwa na Khatimu Naheka baada ya beki wa NSSF, kumchezea rafu mbaya Shadraki Kilasi aliyekuwa anakaribia kufunga.  Katika mchezo, Taswa  Fc ingeweza kusawazisha na kama si kukosa penati kwa mshambuliaji wa Taswa FC, Saidi Seifu ambaye kipa wa NSSF aliipangua.

Penati hiyo ilitolewa baada ya beki wa kati wa NSSF kumwangusha Zahoro Mlanzi aliyecheza vizuri na mshambuliaji wa pembeni wa timu Taswa FC Angetile Osiah ambaye pia alikosa mabao mawili ya wazi baada ya kupiga mpira nje.

Mbali ya Osiah, Seif, Julius Kihampa na Mohamed Akida nao walikosa nafasi nyingi za wazi katika mechi hiyo ambayo wachezaji, Wilbert Molandi, Nurdin Mponda, Jabir Johnson na Simon walicheza vizuri sana.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa hawajaridhika na kipigo hicho cha mara ya kwanza tokea kuanza kwa mwaka huu na kujipanga upya kwa ajili ya mechi ya marudiano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...