Mgombea
Urais kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya
wananchi wa Sengerema jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini
humo.Katika mkutano huo wa kampeni Dkt Magufuli amezishauri halmashauri nchini
kuacha tabia ya kukopa pesa kutoka katika taasisis za kifedha na kulipia fidia
za wananchi ambapo serikali inataka kutumia maeneo yao kwa ajili ya huduma za
kijamii.
Akiomba kura
katika wilaya mpya ya Nyang'wale mkoani Geita,Dkt Magufuli ametumia jukwaa hilo
kukataza mpango wa kukopa pesa kutoka kwa taasisi za kifedha,ambapo wamekua
wakitaka riba kubwa ili kuweza kulipa fidia kwa wakazi ambao wameamishwa
kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za halmashauri hiyo mpya ya Nyang'wale kwa kutaka
kutafutwa kwa njia nyingine za upatikanaji wa fedha hizo kupitia mapato yao.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana na mkazi wa Sengerema
aliposimama kuwasalimia wananchi alipokuwa akielekea kwenye mkutano wa
kampeni.
Mkuu
wa msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Ndugu Abdallah Bulembo
akitoe maeleoz mafupi kwa wakazi wa Nyang'wale namna ya kuwapigia kura
wagonbea wa CCM.
Mgombe
Urais wa CCM Dkt John Magufuli
akiwanadi madiwani wa wilaya ya Sengerema mbele ya maelfu ya wananchi
alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni,ambapo
aliwaomba wampigie kura za kutosha ili aibuke mshindi na kuwa rais wa
awamu ya tano
Wakazi
wa mji wa Sengerema wakimsikiliza Mgombe Urais wa CCM Dkt John Magufuli
alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni,ambapo
aliwaomba wampigie kura za kutosha ili aibuke mshindi na kuwa rais wa
awamu ya tano.
Wananchi wakiwa wamefunga njia wakitaka Mgombea Urais wa CCM Dkt
Magufuli awasalimie na pia wamweleze shida zao,ili iwapo akichaguliwa
katika nafasi ya Urais baasi aweze kuwakumbuka na kuwasaidia.
Msafara
wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya
chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiingia kwenye kivuko
cha Mv Misungwi katika feri ya Busisi akitokea wilayani Sengengerema
kuelekea jijini Mwanza baada ya kumaliza mikutano yake ya kampeni
aliofanya katika wilaya ya Geita vijijini,wilaya ya Nyang'wale pamoja na
Sengerema mkoani Mwanza.
Endeleza kampeni unakaribia utepe wa mwisho. Tunakuunga mkono
ReplyDelete