Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa jimbo la Chalinze,Ndugu Ridhiwani Kikwete.Dkt Magufuli amefanya mikutano ya kampeni katika jimbo la Kawe,Chalinze,Kibaha vijijini,Kibamba na Kibaha mjini.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi kitabu cha Ilani ya ccm kwa Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha vijini .Nduggu Hamoud Abuu Jumaa.
Mmoja wa wafuasi wa CHADEMA alipojichanganya kwenye mkutano wa CCM,maara baada ya kuvutiwa na sera za Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akijinadi mbele ya wananchi.
 Umati wa wakazi wa jimbo la Kawe wakifuatilia mkutano wa kameni
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa-CCM,Dkt Gharib Bilal akimuombea kura za ushindi Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Bunju jioni ya leo jijini Dar.
 Sehemu ya umati wa watu wakiwa wamekusanyika viwanja vya Bunju,kwenye mkutano wa kampeni jimbo la kawe jioni ya leo ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alijinadi na kuomba kura za ushindi ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

 Sehemu ya umati wa wakazi wa jimbo la kawe wakishangilia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Bunju jioni ya leo jijini Dar
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kawe,Keppy Warioba viwanja vya Bunju jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wa jimbo la Kawe wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Bunju,jijini Dar
Wanachama wa CCM wakishangilia kwa staili ya namna yake,kwenye mkutano wakampeni mjini Kibaha.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Astaghfirullah. Maana inanibidi kwanza nistaghfiru kuona hilo jeneza la 'R.I.P UKAWA 2014-2015.
    Well, nnachotaka kunena ni kuzidi kuiombea AMANI, UMOJA, UTULIVU na USALAMA nchi yetu hii ya TANZANIA na raia wake wote, ndani na nje ya nchi. Mwenyeez Mungu atujaaliye kama alivyotujaalia kuwa na kampeni za amani, utulivu na salama. Kadhalika atujaaliye hilo ifikapo na siku rasmi ya uchaguzi mkuu iwe ni yenye kugubikwa na wingu la AMANI, UMOJA, UTULIVU na USALAMA tangu mwanzo wa zoezi zima la upigaji kura hadi kumalizika kwake na mpaka kutangazwa rasmi kwa matokeo yake.

    Naamini kabisa, endapo hilo tutalizingatia (Amani, umoja, utulivu na usalama), basi naamini Tanzania itakuwa ni nchi moja ya kupigiwa mfano wa pekee ndani na nje ya nchi, kwa kudumisha amani ya nchi yake, khususan katika kipindi hiki cha kampeni na mpaka kumalizika kwa chaguzi zetu mbali mbali nchini na hadi kufikia khatma yake na kutangazwa kwa matokeo yake. Hivyo ni wajibu na jukumu la kila mtanzania ndani na nje ya nchi, kuilinda na kuidumisha amani iliyopo, umoja wetu, utulivu na mshikamano wetu pamoja na kuudumisha usalama wa nchi yetu. Tusisahau, maisha si kipindi cha kampeni na uchaguzi tu, hayo ni ya kupita, bali kuna maisha mengine pia baada ya kulikamilisha zoezi hilo. MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE, IBARIKI AFRIKA NA DUNIA KWA JUMLA - AMEN.

    ReplyDelete
  2. Na wachadema ruksa mumuunge mkono mgombea wetu wa CCM. Magufuli oyeeee, Tanzania oyeeee. Tupige kura kwa amani tumuunge mkono rais ajaye. Vyama visiruhusiwe kuharibu umoja wa watanzania.Uzuri wa mchanganyiko huu ni ushindi wa Tanzania.

    Mgombea urais atakayeshinda bara anapata dhamana ya kutawala (winner takes all) akiamua kama awamu ya nne akakumbuka kumteua angalau mmoja au wawili wa upinzani.

    Wenzetu wa Zanzibar kwenye serikali ya kitaifa atakayeshinda wanagawana mkate nusu kwa nusu (win win) kwa vyama vikuu wiwili vya visiwani.

    CCM Oyeeeee. Tanzania oyee.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...