Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa CCM na Mwenyekiti wa kamati ya kampeni za chama hicho,Ndugu Abdulrahman Kinana wakiwasalimia wakazi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake kabla ya kuanza kwa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha
Mgombea Ubunge wa jimbo la Simanjiro na Mjumbe wa kamati ya ushindi ya kampeni za CCM,Ndugu Ole Sendeka akiwahutubia maelfu a wananchi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha.
Katibu Mkuu wa CCM na Mwenyekiti wa kamati ya kampeni za chama hicho,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia maelfu ya wananchi wa jiji la Arusha na vitongoji vyake,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid,mkoani Arusha.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Monduli,Namelok  Edward Moringe Sokoine kwenye mkutano wa kampeni ulofanyka mjini Monduli mapema leo mchana.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM Mgombea Ubunge wa jimbo la Arusha mjini,Ndugu Phillemon Mollel mbele ya maelfu ya  wakazi wa jiji la Arusha kwenye mkutano wa kampeni
Baadhi ya Wanachama wa Chadema wakirejesha kadi zao kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo jijini Arusha
Umati wa Wakazi wa jiji la Arusha na Vitongoji vyake wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakati wa Kampeni za Kumnadi Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt John Pombe Magufuli jijini humo.
Wananchi wa Arusha waliofurika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid wakionesha kufurahia Sera za Chama cha Mapinduzi CCM wakati wa Kampeni za Kumnadi Mgombea Urais wa Chama hicho Dkt John Pombe Magufuli.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tunataka video ili tusikie na kuchambua sera. Ningependekeza katika kila campain stop: mfano, Haydom, mbulu, Arusha mjini etc. kuwe na picha kadhaa na video yake. Hiyo itasaidia sana kunadi sera za wagombea hata kwa walioshindwa kuhudhuria mikutano.

    ReplyDelete
  2. Kweli hata Idd Amin alikuwa na mashabiki wake. Naona mmeamua kutoonyesha jinsi mkutano wa Monduli ulivyojaa watu. Safari hii mmenoa. Tafute kazi nyingine za kufanya baada ya Oct 25. Wananchi wamekwishaamua hivyo.

    ReplyDelete
  3. Mbona wataisoma ?

    ReplyDelete
  4. hapa ni kazi tuu, uwiii safiiiiiiiiii sana

    ReplyDelete
  5. CCM endelea kusongambele.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...