![]() | ||
Mh. Magufuli Akimnadi Mgombea ubunge wa Moshi Mjini Mh. Davis Elisa Mosha. |
Mkutano wa Kampezi za Mgombea Urais Kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro umerindima jana katika Jimbo la Moshi mjini katika Viwanja vya Mashujaa na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa CCM wa Wilaya, Mkoa na Kitaifa.
Mbali na Mgombea Urais kupitia Tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli alikuwepo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya ccm na Mlezi wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndhugu Emanuel Nchimbi, pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Simanjiro Mh. Ole Sendeka.
Akizungumza na Wakazi wa Moshi Mjini Mh. Ole Sendeka aliwasihi wanachama wa CCM na wapenzi wa CCM kuepukana na kuwajibu wanachama na Wafuasi wa Vyama vinavyounda ukawa kwa sababu Ukawa wamedhamiria kuchokoza wana ccm ili kutokee machafuko ili ionekane ni CCM ndio wameleta vurugu.
Akizungumza na wakazi wa Moshi, Mgombea Urais Dkt. John Pombe Magufuli alimzungumzia Mh. Davis Mosha kuwa hana shaka naye kwani anaelewa ni Mchapakazi na Mtekelezaji. Amekua mmoja wa Vijana wa kitanzania wenye mafanikio Makubwa kwa kuwekeza vyema katika nchi yetu ya Tanzania. Mh. Magufuli alimuahidi Ndugu Mosha kilometa kumi ya lami ndani ya Jimbo la Moshi mjini iwapo tu wana Moshi watamchagua.
“Davis Aliniambia kuwa Moshi ina maeneo Mengi Muhimu ambayo Barabara zake sio kiwango cha Lami, Na mimi namuahidi Nitamletea Kilometa kumi za Barabara ndani ya Moshi Mjini”
Alisema Mh. Magufuli huku Akishangiliwa na Umati mkubwa wa watu.
Mh. Davis Mosha aliwaasa wananchi wa Moshi Mjini wasifanye makosa na kuwaambia huu ni wakati wa maendeleo na Moshi Mjini itajengwa na watu wa Moshi hivyo wampatie Kura za Urais kwa Dr. John Pombe MAgufuli na Kura za Ubunge kwa Davis Mosha huku Madiwani wapewe wa Chama cha Mapinduzi ili kuweza kufanya kazi kwa Pamoja ya Maendeleo ya Moshi Mjini.
Wagombea na viongozi mbalimbali wakiimba wimbo maalumu wa Amani na Umoja. |
Mh. John Magufuli akizungumza na Halaiki ya watu mjini Moshi. |
![]() |
Halaiki ya watu katika mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais na Ubunge wa CCM. |
![]() |
Mh. Davis Mosha Mwenye shati la njano wapili kulia akiongoza Madiwani wake katika zoezi la Nguvu na Afya. |
Mh. Davis Mosha akiwa na Wakereketwa wa ccm Moshi Mjini |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...