Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Profesa Adolf Mkenda ( wa pili kushoto ) akimkabidhi cheti Msafiri Mpendu muda mfupi mara baada ya kufunga ya siku tatu yaliyolenga kujenga uelewa juu ya mpango wa serikali wa kushirikisha sekta binafsi kushiriki katika miradi mikubwa kupitia ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (kushoto ) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini Godfrey Simbeye, ( wa tatu kushoto ) ni Kamishna wa PPP Frank Mhilu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Bw.Godfrey Simbeye akisisitiza jambo kwenye mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uelewa wajasiriamali wakubwa na wakati juu ya mpango wa serikali wa kushirikisha sekta binafsi kushiriki katika miradi mikubwa kupitia ubia kati ya sekta ya umma na binafsi ( PPP) mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki ya Dunia yalifungwa jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...