Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal akihutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akizungumza kwenye mktano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar
Dogo Aslay akitumbuiza wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo Kibandamaiti mjini Zanzibar.
Mgomea Mwenza wa Urais kwa tikei ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kufunga kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Kibanda maiti mjini Zanzibar. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).
Si haba Alhamdulillah! Hatimae zoezi zima la kampeni limefikia tamati yake. Pole sana Mama Samia Suluhu, kwa kuiranda takriban Tanzania nzima, bara na visiwani kukinadi Chama tawala na upigaji wa kampeni kwa jumla, haikuwa kazi rakhisi lakini mmeweza kuifanikisha shughuli hiyo. Hata hivyo kazi bado haijesha, iliyopita ni mithli ya 'bashraf' khabari kamili ni hiyo siku ya siku panapo uhai na uzima In Sha Allah. Naamini kwa umati uliojitokeza katika mikutano yote ya kampeni na jinsi unavyojionyesha hapo, tayari ni ushindi mkubwa kwa Chama tawala nikimaanisha Mh. John Pombe Magufuli na mgombea mwenza Bi Samia Hassan Suluhu. Kila la kheri na uwe uchaguzi wa salama, amani na utulivu kwa vyama vyote ifikapo hiyo siku ya siku. Kwa Chama tawala naamini hakuna la ziada, mambo yote ni kuMAGUFULIka tu kwani 'HAPA KAZI TU'
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI TANZANIA, IBARIKI AFRIKA, IBARIKI DUNIA NZIMA KWA JUMLA - AMEN.
Hapa kazi 2
ReplyDeleteTanzania oyee, Tumalize uchaguzi kwa amani, wataoshinda kura tuwapongeze, wataoshindwa wasikate tamaa waendelee kuchangia maendeleo ya nchi, uchaguzi ujao wajitose tena. EE MUNGU IBARIKI TANZANIA, NA WATANZANIA WOTE.
ReplyDelete