Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo umesaini mkataba na Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu nchini (TFF) wa kuwa mdhamini rasmi wa bima za afya kwa vilabu vya ligi kuu ya Vodacom nchini. 
 Akizungumza wakati wa kutia saini mkataba huo Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Rehani Athumani, amesema katika udhamini huo utakaodumu kwa mwaka mmoja NHIF itakuwa inatoa huduma za matibabu kwa wachezaji na benchi la ufundi kwa klabu zote 16 za ligi kuu, huduma ambazo zitapatikana katika vituo vya matibabu zaidi ya 6100 vilivyosajiliwa nchini kote. 
 Amesema lengo la NHIF katika mkataba huo ni kuona kuwa wachezaji wa mpira wa mguu nchini kwa kuanzia na ligi kuu wanakuwa na uhakika wa matibabu ndani na nje ya uwanja. Bwana Rehani ameongeza kuwa kwa vile hivi sasa mchezo wa mpira wa miguu unachukuliwa kuwa kama ajira, ni vema wachezaji wakahakikishiwa usalama wa afya zao wawapo uwanjani na nje ya uwanja hali itakayowafanya wajiamini zaidi katika mchezo. 
 Amesema NHIF imeandaa utaratibu maalumu wa kutoa elimu ya afya, lishe na saikolojia kwa vilabu vyote 16 ili kuhakikisha kuwa wachezaji wanakuwa katika hali nzuri ya kiafya kimwili na kiakili. Naye Katibu Mkuu wa TFF Bwana Mwesiga Celestine ameelezea matumaina yake kuwa hatua ya NHIF kudhamini vilabu vya ligi kuu itasaidia kuinua kiwango cha soka nchini na kuirejesha Tanzania katika ramani ya nchi zinazofanya vizuri katika mchezo huo. 
 Aidha amewaomba wadau wengine kutoa udhamini kama huo kwa madaraja mengine ili kuwapa hamasa wachezaji wa madaraja hayo. Akizungumza kwa niaba ya vilabu vya ligi kuu ya Vodacom, mwakilishi wa vilabu Bwna Jerry Muro amesema udhamini wa NHIF umekuja kwa wakati muafaka kwani vilabu vingi vimekuwa vikishindwa kuhudumia wachezaji wao ipasavyo wakati wanapougua au kupata majeraha kutokana na gharama kubwa ya matibabu. 
 Amesema hatua ya NHIF kubeba dhamana ya kuhudumia wachezaji katika sualala afya itasaidia sana kuinua viwango vya soka nchini kwa kuwa wataingia viwanjani wakiwa wanajiamini. 
 Muro ameishukuru TFF kwa kuingia katika mkataba huo ambao unavinufaisha vilabu moja kwa moja na kuahidi kutoa ushirikiano wa asilimia mia moja kwa wadau hao wa afya.
 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Athumani Rehani akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kusaini mkataba wa huduma za matibabu kwa wachezaji wa  Shirikisho la vyama vya mpira wa Minguu Tanzania (TFF) leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shilikisho la mpila wa Minguu Tanzania (TFF)  Mwesiga Celestine
 Mwakilishi wa Mkurungenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Athumani Rehani na kulia Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF)  Mwesiga Celestine wakisani mkataba huo
 Katibu Mkuu wa Shilikisho la mpira wa Miguu Tanzania  (TFF)  Mwesiga Celestine akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kuupongeza uongozi mzima wa (NHIF) kwa kusaini mkataba  huo. Kulia kwake ni Mwakilishi wa Mkurungenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Mkurungenzi wa Masoko na Utafiti Athumani Rehani 

 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Athumani Rehani (kushoto) akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa NHIF  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano   wa Club ya Yanga Jerry Muro. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa Minguu Tanzania  (TFF)  Mwesiga Celestine.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Athumani Rehani akiwa katika bicha ya pamoja na viongozi Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania  (TFF)  Pamoja na maofisa wa (NHIF). Picha na habari na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...