IMG_9939
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda wakati wa ziara fupi ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kukomesha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea Dawati la jinsia la Wanawake na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda alisema umoja huo umelenga kusaidia uwepo wa utawala wa sheria na wenye kujali haki na utu wa binadamu kupitia mpango mkakati wake uliomo katika malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kuanzia mwaka 2016 utakosaidia kuondoa vitendo hivyo.

Alieleza kuwa tatizo la udhalilishaji wa kijinsia sio kwa Zanzibar pekee bali ni la kidunia, hivyo umoja wa mataifa(UN) unawajibu kusaidia juhudi za serikali kupambana na tatizo hilo.

“Tushirikiane kwa kila hatua ili kuondosha vitendo hivi kwani ni tatizo na kero kwa jamii ya Zanzibar pia ni miongoni mwa ishara tosha zinazoashiria uvunjifu wa haki za binadamu.”, alisema Rodriguez na kusisitiza kuwa ili kukomesha vitendo hivyo ni kuwepo na utawala wa kisheria utakaotenda haki kwa wale wanaoozalilishwa utu wao.
IMG_9951
Aidha Bw. Rodriguez aliyataka madawati ya jinsia kutumia vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ili kuhakikisha vinapungua ama kuisha kabisa kwa lengo la kujenga jamii yenye uadilifu.

Naye Mtendaji wa Dawati hilo, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma alifafanua kuwa kesi za ubakaji kwa wanawake na watoto zimepungua ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...