93.7 EFM
inaendeleza burudani kupitia kampeni yake ya muziki mnene Bar kwa Bar. Jumamosi
ilikuwa zamu ya wakazi wa Bunju kuongea
na muziki wa 93.7 EFM.
Burudani hiyo iliendeshwa
na timu nzima ya EFM, iliyocheza mechi na Carlfonia FC ya Boko na kuwafunga magoli mawili kwa moja katika uwanja
wao wa nyumbani uliopo ndani ya shule ya msingi Boko. “Kwa bahati mbaya
tumeshafungwa mechi tatu ila kuanzia mechi hii ni mwendo wakufunga magori ya kishujaa”
alisema Dennis Ssebo mkuu wa idara ya mahusiano na mawasiliano.
Baada ya mechi
hiyo shangwe ziliendelea ndani Rainer park Boko huku Rdjs wa 93.7 Efm wakitoa
burudani ya aina yake iliyo acha historia
kwa wakazi wa Boko.

Wachezaji wa 93.7 EFM na Carlfonia FC ya Boko wakisakata kabumbu katika uwanja wa shule ya msingi boko.
Baadhi ya mshabiki waliojitokeza kushabikia mechi kati ya EFM na Carlfonia FC oko.
Rdj X5 na Rdj timber wakifanya kazi yao kwa umakini.
Wakazi wa Bunju wakifurahia burudani ndani ya Rainer park Bunju.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...