ASKALI Polisi wa mjini Babati, Mkoa wa Manyara ameuawa kwa kuchomwa kisu na mtangazaji mmoja wa redio kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Baadhi ya wakazi wa Babati walisema jana kuwa wanaume hao walikuwa wakimgombea mwanafunzi wa kidato cha pili walipokuwa baa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime alimtaja aliyeuawa kuwa ni Rashid Haruna (30) mwenyeji wa Mkoa wa Njombe.Kamanda Fuime alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5.30 usiku eneo la Kitalu X.

Alisema Polisi wanamshikilia mwanafunzi huyo wakati uchunguzi zaidi kuhusu mauaji hayo ukiendelea.Kamanda Fuime alisema baada ya mtangazaji huyo kumchoma kisu askari huyo alikimbilia sehemu za Dareda.

“Kabla ya kifo chake alichomwa kisu mara 15 sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwamo mikononi, mgongoni, ubavuni na eneo la moyo,” alisema Kamanda Fuime.Kamanda Fuime alisema mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda wilayani Makete Mkoa wa Njombe kwa maziko.

Awali askari ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema siku ya tukio polisi huyo alimkuta msichana baa akiwa analumbana na mtangazaji. 

Alisema msichana huyo alimuomba askari ambaye ni mpenzi wake amsaidie kwani anang’ang’aniwa na mtu asiyempenda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mambo gani haya yasiyothamini maisha kiasi hiki?..

    ReplyDelete
  2. Hii ni aibu kubwa kwa jamii ya Watanzania, kwa sababu inaonyesha wazi jinsi jamii inavyokwenda ovyo ovyo tu, bila kuzingatia, kufundisha na kutekeleza (inforciment} maadili mema kwa watu wake. Siamini kwamba huyu msichana ni mwanafunzi, na kama ni mwanafunzi kweli kweli swali langu ni Je, ktk jamii ya kitanzania wanafunzi wanaruhusiwa kuingia Baa na kustarehe? na Je, watumishi wa Baa husika na Bar zinginezo wanao uwezo wa kumtazama mtu kwa macho na kumtambua kuwa ana umri mdogo hastahili kuingia baa hata angekuwa pande? Kuna maswali mengi tu ya kujiuliza juu ya swala hili.

    Inawezekana kabisa kwamba huyu mwanafunzi haishi na wazazi wake kwa sasa, huenda kapangishiwa chumba na wazazi/walezi ili apate kwenda shule, baadae awe na maisha bora na kuongeza tija ktk taifa letu. Je, Vipi wanajamii wengine/wateja au watumishi wa hiyo baa kwa vipi wasilione jambo la mwanafunzi kuingia katika baa kuwa ni jambo linalovunja maadili yetu mema kwa hiyo wakalikemea au kumthibiti huyo mwanafunzi mapema? Maana tusisahau kwamba katika Afrika yote malezi ya mtoto ni jukumu la jamii yote sio wazazi tu. Vipi watanzania tumelisahau hili jambo jema mno na tukaanza kukumbatia mambo ya wangine kama:Valentine day, birth day, thanks giving, haloween, Mothers/Fathers day,nk! Mbona wao hawajakumbatia yetu hata moja???

    Nirudi kwenya point?mada yetu. Kwa ajili ya kutokuwa makini na kukosa maarifa tumempoteza askari (kwa sababu za kienda wazimu}, mtu muhim sana katika jamii, maana hakuna jamii yeyote inayaweza kuwepo bila askari polisi. Polisi wanaweza kuitwa majina tofauti katika jamii tafauti lakini ikumbukwe kwamba kazi yao ni moja ile ile: Kulinda usalama wa raia na mali zao.

    Sijui mamlaka ya kutoa leseni za baa wanaliona hili!
    Je, wakuu wa Polisi ngazi mbalimbali:, wilaya, mikoa, mpaka Taifa wanaliona vipi!

    Basi nisiseme sana nisije nikakamatwa mimi badala ya muuwaji. Ila
    ukweli inasikitisha sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...