Wachezaji wa timu ya EFM na timu ya Magogoni Veteran katika uwanja wa shule ya msingi Ufukoni.
Wakazi wa kigamboni wakishuhudia mechi kati ya EFM na Magogoni Veteran kigamboni.
Mamia ya watu waliojitokeza kushabikia kabumbu kati ya 93.7 EFM na Magogoni Veteran Kigamboni.
MUZIKI mnene Bar kwa Bar wiki iliyopita ulivuka kivuko na kuhamia Kigamboni,wakazi wa eneo hilo ambao ni wasikilizaji wa 93.7 EFM walipata burudani ya aina yake kutoka kwa timu nzima ya EFM redio.
Burudani
ilianza na kabumbu katika uwanja wa shule ya msingi Ufukoni kati ya EFM na
magogoni veteran,Timu ya magogoni veterani ilitetea ushindi nyumbani kwa
kuifunga EFM magoli manne huku EFM ikiambulia mawili 2.
Kwa kuwa
kigamboni kumezungukwa na fukwe kibao, muziki mnene uliendelea katika fukwe ya
Navy beach. Rdj’s walishusha ngoma kali na kuwapagawisha wakazi wa kigamboni
kwa burudani ya kihistoria.
Baada ya pwani ni zamu ya Dar-es-salaam hivo wakazi wa jiji hili
wajiandae kwa kuwa tutawafikia na kuwapa burudani ya kihistoria alisema Denniss
Ssebo mkuu wa idara ya mahusiano EFM.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...