Mkurugenzi wa NMB - Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.
Wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (Tanzania Editors Forum) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) jijini Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya miaka 10 ya benki hiyo tangu ilipobinafsishwa na hatua ilizopiga katika maendeleo ya benki.
BENKI ya NMB jana ilianza maadhimisho ya miaka 10 tangu kubinafsishwa huku ikiweka bayana mafanikio makubwa iliyoyapata ikiwemo kuongeza matawi kutoka chini ya 100 miaka 10 iliyopita mpaka matawi 173 leo hii, kutoka kutokuwa na ATM mpaka ATM zaidi ya 600 na wateja kufikia zaidi ya milioni 2 kutoka laki 6 miaka 10 iliyopita.
NMB pia imefanikiwa kuwa na matawi katika kila wilaya nchini. Hii inaonesha ni jinsi gani Benki imekuwa kwa kasi na kuwa benki namba moja kwa ukubwa na faida kuliko benki nyingine yoyote nchini Tanzania.
Kwa miaka 10 pia NMB imetumia zaidi ya shilingi Bilioni 7 kusaidia shughuli za maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia madawati mashuleni, vifaa vya hospitali katika hospitali mbalimbali za serikali huku ikichangia kuongeza ufanisi wa utoaji huduma katika sekta ya afya na elimu.
NMB Pia imechangia zaidi ya Bilioni 365 ndani ya miaka 5 tu fedha ambayo imechangia sana kwenye bajeti ya serikali na hivyo kutumika kwa maendeleo ya watanzania. Huo ni mchango mkubwa kuliko benki yoyote nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...